Home VIWANDAMIUNDOMBINU Italia yaahidi kuisaidia Tanzania mradi wa SGR

Italia yaahidi kuisaidia Tanzania mradi wa SGR

0 comments 14 views

Waziri wa Fedha,  Dkt. Mwigulu Nchemba  ameishukuru Italia kwa kutoa dhamana ya mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Kwanza na cha pili kuanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Makutupora mkoani Singida, ambavyo ujenzi wake umekamilika na treni imeanza kutoa huduma kuanzia Dar es salaam hadi Dodoma.

Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo mjini Rome nchini Italia, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia ( SACE),  Alessandra Ricci.

Alieleza kuwa kutokana na mchango huo, SGR imeanza kutoa huduma ya kubeba abiria kuanzia Julai mwaka 2024, ikiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya usafiri nchini, ambapo muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma umepungua kutoka saa nane hadi takriban saa tatu.

Aidha, Waziri Nchemba alieleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini nia njema ya SACE kuendelea kudhamini ujenzi wa reli toka Dodoma hadi Isaka

Aidha, Dkt. Nchemba aliwaalika wawekezaji kutoka Italia kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa miundombinu ya reli pamoja na ujenzi wa viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa nchi wa pande hizo mbili.

Alisema kuwa Tanzania iko katika eneo zuri la kimkakati kijiografia kwa kupakana na nchi 6 zisizopakana na Bahari na zinazotegemea Bandari ya Dar Es Salaam, hatua ambayo inalifanya eneo lote la nchi na nchi jirani kuwa soko zuri na la ukakika la bidhaa na huduma na kuishauri sekta binafsi ya nchi hiyo kuchangamkia fursa hizo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia, SACE, Alessandra Ricci, alisema kuwa Italia imeichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 14 za Afrika zitakazonufaika na usadizi wa kifedha kutoka nchi hiyo kutokana na uhusiano mzuri wa kiuchumi uliopo kati ya nchi hizo mbili kupitia Mpango wake wa Ushhirikiano kati ya Italia na nchi za Afrika ujulikanao kama Piano Mattei.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia ( SACE), Alessandra Ricci.

Ricci aliahidi kuwa Shirika lake liko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kugharamia mradi wa SGR kipande cha 3 na 4. kinachoanzia Makutupora mkoani Singida -Tabora hadi Isaka, kutokana na umuhimu wa mradi huo katika kukuza biashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!