Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mchakato ujenzi barabara Igawa-Tunduma waanza

Mchakato ujenzi barabara Igawa-Tunduma waanza

0 comment 115 views

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema wataalamu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wameanza mchakato wa upembuzi yakinifu wa ujenzi wa barabara ya Igawa-Tunduma. Chalamila ameeleza kuwa hivi sasa, timu ya wataalamu hao inaendelea na zoezi hilo huku akiongeza kuwa, ujenzi huo unatarajia kutumia muda wa takribani miezi 14.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo wakati akifafanua kuhusu hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kutatua changamoto za miundombinu ya barabara.

“Tayari ujenzi wa barabara kipande cha Igawa hadi Mafinga kimekwisha kamilika,  kwa hiyo hata hii ambayo imeanza kufanyiwa upembuzi nayo itakamilika kwa wakati “. Amesema Chalamila.

Mbali na ujenzi wa barabara ya Igawa-Tunduma, Mkuu huyo pia ameeleza kuwa mchakato wa ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Inyara-Mbalizi maalum kwa ajili ya matumizi ya magari makubwa ya mizigo unaendelea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter