Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mji mpya wa serikali mbioni kukamilika

Mji mpya wa serikali mbioni kukamilika

0 comment 133 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema ujenzi wa mji mpya wa serikali eneo la Mitumba jijini Dodoma umekamilika kwa asilimia 99. Majaliwa amesema hayo wakati wa ziara yake mjini humo ambapo ameeleza kuridhishwa na hatua za ujenzi hadi sasa na kwamba dhamira ya Rais John Magufuli kujenga upya mji wa serikali imetekelezwa.

Pia katika ziara hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliyeambatana na Waziri Mkuu amesema Sh. 50 bilioni zimewanufaisha wakandarasi pamoja na wananchi wa hali ya chini kiuchumi kutokana na uwekezaji mkubwa katika eneo hilo na vilevile uwepo wa biashara ndogondogo kama mama lishe

Hadi sasa, majengo ya wizara 20 tayari yameshakamilika na Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhakikisha hadi kufikia Aprili 15 mwaka huu, kazi iliyosalia ya kuboresha mazingira ya nje ya ofisi hizo inakamilika. Pamoja na hayo, Majaliwa amemuongezea mkandarasi muda wa siku kumi kukamilisha ujenzi wa ofisi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambayo bado haijakamilika hadi sasa.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alibainisha kuwa ujenzi wa mji huo ulioanza rasmi Desemba mwaka jana utakamilika hadi kufikia Februari 2019 lakini muda uliongezwa na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Mei mwaka huu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter