Home VIWANDAMIUNDOMBINU Pemba yajipanga kujenga Uwanja wa Ndege

Pemba yajipanga kujenga Uwanja wa Ndege

0 comment 102 views

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe amesema wizara hiyo imewekeana saini na Kampuni ya Daral Handasah Consultant Limited ya Misri ili kuanza mradi wa upambuzi yakinifu, usanifu na utayarishaji wa zabuni za ujenzi za Uwanja wa Ndege wa Pemba.

Jumbe amesema kuwa awamu ya kwanza ya mradi huo itachukua miezi takribani kumi kukamilika huku awamu ya pili ambayo ni utayarishaji mpango mkuu wa viwanja vya ndege vya Zanzibar pamoja na matumizi bora ya ardhi kwenye uwanja wa Abeid Karume ikichukua kipindi cha miezi tisa.

Mbali na hayo, Katibu huyo ametaja maeneo ambayo yataenda sambamba na mradi huo kama vile mfumo wa zimamoto na uokozi, jingo la kufanyia matengenezo ya ndege, sehemu ya mizigo, maegesho kwa ujumla na uzio wa kiusalama. Ameongeza kuwa mradi huo utagharimu zaidi ya bilioni nne ambayo itakuwa ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AFDB) kwa kupitia serikali ya Tanzania.

Moja ya faida za mradi huo kutokana na maelezo ambayo Katibu Jumbe ametoa ni kwamba, kunakuwa na uelewa wa mahitaji ya kifedha na yale ya kiufundi hivyo kupelekea serikali kutafuta fedha za ujenzi huo ikiwa na uhakika wa kazi ambazo zinatakiwa kufanyika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter