Home VIWANDAMIUNDOMBINU Sababu ya serikali kuipa dili Sicpa

Sababu ya serikali kuipa dili Sicpa

0 comment 93 views

Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango amesema serikali imetoa zabuni ya mradi wa stempu za kielektroniki (ETS) kwa kampuni ya Sicpa kutoka Uswisi kwa sababu Tanzania haina teknolojia ya kumudu kuzitengeneza.

Dk. Mpango amesema hayo wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya serikali bungeni Dodoma ambapo amedai japokuwa serikali ilishauriwa na Kamati ya Bunge pamoja na baadhi ya wabunge kutengeneza mfumo huo wa ETS wenyewe, serikali iliamua kutangaza zabuni ya kimataifa ka uwazi kwani hakuna kampuni wala taasisi ya serikali hapa nchini yenye uwezo wa kutengeneza mfumo huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Hawa Ghasia amesema fedha zinazotarajiwa kuwekezwa na kampuni ya Sicpa ni Dola za Marekani 21,533,827, ambazo ni sawa na Sh. 48.5 bilioni za Tanzania.

Mfumo wa ETS unamtaka mwekezaji kurudisha gharama zake kwa kutoza stempu ya kielektroniki kwa kila bidhaa itakayozalishwa. Kwa makadirio, Sicpa itakusanya takribani Sh. 66.7 bilioni ndani ya mwaka mmoja, kiasi ambacho kimedaiwa kuwa ni kikubwa kuliko kile walichowekeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter