Home VIWANDAMIUNDOMBINU Serikali kumaliza changamoto ya majisafi nchini

Serikali kumaliza changamoto ya majisafi nchini

0 comment 84 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema serikali imedhamiria kumaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa kuchimba visima na kutumia maji kutoka kwemye maziwa na mito na kuyapeleka maeneo mbalimbali ya wananchi nchini. Majaliwa amesema hayo alipozungumza na wananchi wa kata ya Nzera wilayani Geita, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Geita.

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa shule Sekondari Bugando, Waziri Majaliwa amewataka wakuu wa wilaya kusimamia uhifadhi wa maeneo yenye vyanzo vya maji ili kuhakikisha yanaendelea kuwa chepechepe ili vijiji vyote viweze kupatiwa maji ya uhakika.

Waziri Mkuu ameeleza kuwa, serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji safi karibu kabisa na makazi yao kupitia kampeni ya Rais Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani na kuongeza kuwa serikali itahakikisha kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama.

Aidha, Waziri Mkuu amesema pamoja na huduma ya maji, serikali imepanga kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo, ambapo ameeleza kuwa vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA III).

 

 

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter