Home VIWANDAMIUNDOMBINU SGR awamu ya kwanza kukamilika 2019

SGR awamu ya kwanza kukamilika 2019

0 comment 138 views

Mkuu wa Mipango wa kampuni ya Yapi Merkezi, Enis Eryilmaz amesema ujenzi wa awamu ya kwanza wa reli ya kisasa (SGR) umefikia asilimia 16 na unatarajiwa kukamilika Novemba 2019. Eryilmaz amesema hayo katika eneo la Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati wa ziara ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB).

Eryilmaz amesema kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilomita 300 kitakuwa na vituo sita vya Dar es salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro.

“Tumejipanga kumaliza mradi ndani ya wakati, tunatumaini tutasherehekea uzinduzi Novemba 2019.” Amesema mtaalamu huyo.

Eryilmaz ameeleza kuwa, kampuni imeajiri watu 4000 na asilimia 90 kati ya hao ni watanzania.

“Tunajitahidi kufanya kazi bega kwa bega na watanzania ili tukiondoka waweze kuendesha mradi huu na kufanya matengenezo mengine.”Alisema

Meneja Mradi Msaidizi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja amesema reli hiyo itakuwa na kituo cha kupoza umeme kila baada ya kilomita 50 na Shirika la Umeme (TANESCO) litaweka umeme maalum kwa ajili ya reli hiyo. Dar es salaam itakuwa na treni maalum kwa abiria na watajenga kituo kikubwa eneo la Pugu kwa ajili ya abiria wa Dar es salaam na waendao mikoani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter