Home VIWANDAMIUNDOMBINU Tanga Uwasa yalamba ruzuku ya mabilioni

Tanga Uwasa yalamba ruzuku ya mabilioni

0 comment 111 views

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly amesema mamlaka hiyo imefanikiwa kupata ruzuku ya zaidi ya Sh. 1.2 bilioni kufuatia kutumiza masharti ya mkopo wa zaidi ya Sh. 3 bilioni kutoka CRDB kwa lengo la kutekeleza huduma ya majisafi jijini humo. Ruzuku hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani ikiwa mamlaka husika imetimiza masharti ya mkopo huo ikiwa ni pamoja na zoezi la marejesho na kuzingatia suala la utekelezaji wa mradi uliopatiwa fedha hizo.

Mhandisi Hilly amesema mkopo huo kwa kiasi kikubwa umewasaidia kuongeza uwezo wa kusambaza maji hasa katika maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu, hali iliyochangiwa na udogo wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.

“Kama nilivyoonyesha kwamba tumeongeza bomba kubwa la inchi 8 kwa ajili ya kuongeza mgawanyo wa maji kwenye eneo la Neema na kwengineko na kuwepo kwa usambazaji mkubwa kwenye maeneo hayo lakini pia tumejenga mtandao wa Km. 60 kwa kutumia mkopo huo na ruzuku tuliyopewa. Ameeleza Mhandisi huyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Mijini kutoka Wizara ya Maji Dodoma, Mhandisi Lydia Joseph amesema asilimia kubwa ya mamlaka zimekuwa zikilenga kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwa miundombinu iliyojengwa na serikali tangu zamani na kuwepo kwa muda mrefu, hivyo kufuatia ongezeko la watu na mahitaji yao, Mamlaka zinatakiwa kupanua huduma zao ili kuendana na mahitaji halisi ya jamii. Mhandisi Lydia pia ametoa wito kwa mamlaka za maji kuboresha miundombinu ili kuendana na kasi ya ongezeko la watu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter