Taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA) imeingia makubaliano na Sekretarieti ya usafirishaji ukanda wa kati (Central Corridor) na kutoa msaada wa Sh. 2.86 bilioni ambazo zitatumika kutatua changamoto za usafirishaji.
Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkazi wa TMEA John Ulanga amesema kuwa taasisi hiyo imetoa msaada huo ili kuunga mkono jitihada za sekretarieti hiyo katika kutoa data, mapendekezo na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya usafirishaji ambayo inachangia ukuaji wa uchumi kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Central Corridor Kapteni Dieudonne Dukundane amesema fedha hizo ambazo zitatumika hadi mwaka 2021 zitasaidia kujibu maswali ya muda mrefu ya wafanyabiashara na wadau wa usafirishaji kwa ujumla kutoka kwa nchi wanachama