Home KILIMO Wachina wasaini mkataba wa kununua karafuu Zanzibar

Wachina wasaini mkataba wa kununua karafuu Zanzibar

0 comment 44 views

Shirika la Biashara la Zanzibar (ZSTC) limeingia makubaliano ya kuuza mafuta ya karafuu na mkaratusi na kampuni ya Kunshan Asia Aroma kutoka nchini China. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Dk. Said Seif Mzee amesema japokuwa uwezo wao ni kuzalisha tani 60 pekee kwa mwaka, wamejipanga kufikia malengo ya kampuni hiyo kwani wanazo mashine za kisasa za uzalishaji.

Kwa upande wake, Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali ameeleza kuwa kampuni ya Kunshan Asia Aroma imeridhishwa na kiwango kizuri cha bidhaa zinazotoka visiwani humo ndio maana wamefikia maamuzi ya kuingia makubaliano na ZSTC. Zanzibar ni moja kati ya visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora zaidi duniani. Zao hilo linachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Zanzibar hivyo fursa hii ya uwekezaji inafungua milango kwa makampuni zaidi kutoka ndani na hata nje kuwekeza katika zao hili, jambo ambalo litasaidia serikali kupata mapato

Naye Mwenyekiti wa kampuni hiyo, John Zhou amesema kuwa Kunshan Asia Aroma itashirikiana na ZSTC ili kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter