Home VIWANDAMIUNDOMBINU Ukuta wa Mirerani waingizia serikali mamilioni

Ukuta wa Mirerani waingizia serikali mamilioni

0 comment 138 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amesema kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu, serikali imefanikiwa kupata mapato ya Sh. 714 milioni, fedha ambazo zimepatikana miezi mitatu tu tangu ujenzi wa ukuta katika migodi ya madini ya Mirerani mkoani Manyara ikilinganishwa na Sh. 147.1 milioni zilizopatikana katika kipindi chote cha mwaka 2017.

Majaliwa amesema hayo wakati akihitimisha hotuba ya makadirio na matumizi ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 bungeni Dodoma ambapo amesisitiza kuwa ongezeko la mapato limetokana na jitihada zilizofanywa na serikali kuimarisha ulinzi wakati wote wa ujenzi wa ukuta katika migodi hiyo ya tanzanite.

Pamoja na manufaa hayo, Waziri Mkuu pia ametangaza mpango wa kujenga nyumba ambazo zitatumika kama sehemu ya kuuzia madini ili wananchi waishio maeneo ya karibu waweze kufaidika na rasilimali zinazowazunguka.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter