Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika Oktoba 4, 2023 huku bei ya dizeli ikizidi kupaa ikilinganishwa na mwezi Septemba.
Taarifa ya Ewura inasema kwa mkoa wa Dar es Salaam lita ya petrol kwa bei ya rejareja ni Sh3,281, dizeli Sh3,448 na mafuta ya taa yakiuzwa Sh2,943.
Kwa upande wa mkoa wa Tanga lita ya petroli ikiuzwa Sh3,327, dizeli Sh3,494 na mafuta taa Sh2,989.
Aidha Mtwara dizeli imezidi kupaa mara dufu ikiuzwa kwa lita Sh3,520, petroli Sh3,353 na mafuta ya taa Sh3,016.
Ewura imetaja sababu ya mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Oktoba 2023 ikiwa ni kupanda kwa gharama za bidhaa hiyo katika soko la dunia hadi kufikia asilimia 4.21 na gharama za uagizaji kufikia asilimia 17 kwa petroli, asilimia 62 kwa dizeli na asilimia 4 kwa mafuta ya taa.
Nyingine ni uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa mafuta duniani (OPEC+) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya kiuchumi ambavyo nchi ya Urusi imewekewa na mataifa ya magharibi.
Soma: Bei za mafuta zapanda tena Tz