Home VIWANDANISHATI Bilioni 87 kupeleka umeme Kigoma

Bilioni 87 kupeleka umeme Kigoma

0 comment 135 views

Serikali inategemea kutumia Sh. Bilioni 87 kupeleka umeme wa gridi mkoani Kigoma kutoka mkoa wa Tabora. Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amethibitisha hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nkuba kata ya Kasanda, iliyopo wilaya ya Kakonko wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Kigoma.

“Serikali imeona ichukue hatua za haraka kuhakikisha umeme wa gridi unafika mkoani Kigoma katika kipindi kifupi kijacho. Mahitaji ya umeme mkoani humo ni makubwa hivyo hatua za dharura lazima zifanyike sasa kukabiliana na hilo ambapo umeme wa KVA 130 utasafirishwa”. Ameeleza Dk. Kalemani.

Waziri Kalemani ametumia nafasi hiyo kuwaonya wakandarasi ambao wana tabia ya kuruka nyumba za nyasi ambazo zipo kwenye maeneo yanayotakiwa kupata umeme na kuagiza wakandarasi hao kutoa maelekezo katika nyumba zote ili vigezo vizingatiwe.

Wakati huo huo, Wananchi wa kijiji hicho wamemlalamikia Waziri Kalemani kuhusu suala la kutozwa zaidi ya Sh.  150,000 kwa ajili ya nguzo, jambo ambalo limesababisha kuchelewa kupata umeme na kumuomba Waziri huyo kulishughulikia ili waweze kupata huduma ya umeme.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter