Home VIWANDANISHATI Mradi wa bomba la mafuta upo pale pale- Dk. Kalemani

Mradi wa bomba la mafuta upo pale pale- Dk. Kalemani

0 comment 126 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema mchakato wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kuanzia Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga upo pale pale. Dk. Kalemani amesema hayo kwenye semina ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma na kuongeza kuwa makubaliano kati ya Tanzania na Uganda yanaendelea ili ujenzi huo unaokadiriwa kugharimu takribani Sh. 8 trilioni uanze rasmi.

“Tulitarajia majadiliano na serikali ya Uganda yakamilike mwezi huu na hii ni kwa sababu wenzetu waganda walitaka wajihakikishie kuwa baadhi ya waliyogundua, siyo yote ya kusafirishwa, mengine yanatakiwa kusafishwa nchini mwao. Kwa taarifa za mwisho ambazo tunazo ni kuwa Uganda wamekamilisha majadiliano kati yao na mwekezaji wao atakayechimba ili baadhi ya mafuta yasafishwe nchini humo, na hili limechukua muda kidogo kwa wa upande wetu na wao kukamilisha. Matarajio yetu kuanzia mwezi ujao na majadiliano yetu yakamilike na tuanze utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta”. Amesema Waziri Kalemani na kuongeza:

“Najua watanzania walikuwa wanasubiri sana utekelezaji wa mradi huu. Niwahakikishie jitihada za makusudi za viongozi wetu, Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli na Rais Yoweri Museveni ziko pale pale za kutekeleza mradi huu”.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter