Home VIWANDANISHATI Megawati 80 kuingizwa gridi ya taifa

Megawati 80 kuingizwa gridi ya taifa

0 comment 56 views

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limepewa maagizo ya kuingiza kwenye gridi ya taifa megawati 80 kati ya 185 kupitia mradi wa Kinyerezi II unaotegemea kukamilika Agosti mwakani. Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alipotembelea mradi huo eneo la Tabata Kinyerezi jijini Dar es salaam.

Kalemani ameeleza kuwa Megawati 80 hizo zinatakiwa zianze kutumika ili kupunguza changamoto ya ukatikaji wa umeme katika maeneo ya Gongo la Mboto, Kipawa, Kurasini pamoja na Kigamboni na kuchea uzalishaji mali.

“Yani mnaweza kuanza na hizo megawati 80 huku zilizobakia zitakapokamilika mwakani nazo mjitahidi hata kabla ya Agosti ziwe zimeisha ili umeme wa uhakika upatikane na hata kwenye maeneo mengine pia. Serikali inachotaka ni kuona wananchi wanapata umeme wa uhakika ili waongeze nguvu kwenye uimarishaji wa uchumi lakini pia hata wawekezaji nao waendelee kuzalisha zaidi”. Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Meneja wa mradi wa Kinyerezi II Stephen Manda amemhakikishia Dk. Kalemani kuwa megawati hizo zitaingizwa kwenye gridi ya taifa ili zianze kuhudumia maeneo yaliyotajwa.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter