Home VIWANDANISHATI Vijiji 5,000 vyapata umeme

Vijiji 5,000 vyapata umeme

0 comment 86 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Wizara hiyo imefanikiwa kuingia katika rekodi ya dunia kama moja kati ya mataifa machache yanayotekeleza miradi mikubwa ya nishati.

Dk. Kalemani amebainisha hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati, ambapo ameeleza kuwa tangu uhuru wa nchi kupatikana ni vijiji 2,018 ndio vilikuwa vimeunganishwa na umeme ila katika awamu ya tano kwa kipindi cha miaka mitatu vijiji takribani 7,012 vimeunganishwa na nishati hiyo.

“Hii inamaanisha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu vijiji 5000 vimeunganishiwa umeme. Sasa watanzania wanafahamu kuwa umeme ni haki yao ya msingi ndio maana ukienda maeneo hakuna nishati hii basi wananchi watakusimamisha na mabango kuonyesha uhitaji wao”. Ameeleza Waziri huyo.

Pia amesema kuwa serikali inaendelea kupeleka umeme katika vijiji mbalimbali ambapo mwaka 2015 kulikuwa na vijiji 2,000 na mwaka 2018 kulikuwa na vijiji 4,000 ambapo hadi sasa, vijiji 7,012 tayari vimefikishiwa umeme ambayo ni asilimia 240 ya vijiji vyenye umeme kabla ya mwaka 2016.

“Mafanikio hayo ni matokeo ya hatua ngumu za mabadiliko zilizochukuliwa ndani ya Wizara hiyo nyeti kwa lengo la kuleta mageuzi na ufanisi katika kuwahudumia wananchi”. Amesema Waziri Kalemani.

Kuhusu mradi wa gesi asilia, amesema tayari mradi huo umeanza kutekelezwa na tayari baadhi ya viwanda jijini Dar es salaam vimeunganishwa na mradi huo ili kuongeza uzalishaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter