Imeelezwa kuwa bado kuna fursa za ufugaji nyuki ambazo bado hazijatumiwa ipasavyo.
Gilbert Gotifrid ni Afisa Nyuki wa Halmashauri ya Mbinga ambapo anaeleza kuwa kati ya hekta 900 zilizopo katika milima ya Lipembe ambazo zimetengwa kwaajili ya shughuli za ufugaji wa nyuki, ni kama asilimia 1.1 tuu zinatumika kwa shughuli hiyo.
Hii inaonyesha kuwa bado sehemu kubwa iliyotengwa kwa ajili ya ufugaji nyuki haijatumika.
Gotifrid ameeleza kwamba ili kutumia vizuri fursa zilizopo kitengo chake kimekuwa kikitoa elimu kuhusu ufugaji wa nyuki kupitia vipeperushi pamoja na redio zilizopo katika Halmashauri hiyo.