Home BENKI Twiga Bancorp kuendeleza huduma kwenye matawi yao

Twiga Bancorp kuendeleza huduma kwenye matawi yao

0 comment 41 views

Siku moja baada ya Benki kuu ya Tanzania (BoT) kutangaza kuziunganisha Benki ya Posta Tanzania (TPB) na Twiga Bancorp, Ofisa Mtendaji wa TPB Sabasaba Moshingi ametangaza kuwa wateja wa Twiga Bancorp wataendelea kupata huduma katika matawi yao kwa muda wa miezi mitatu wakati zoezi la uunganishaji wa mifumo likiendelea. Moshingi ameeleza kuwa baada ya kipindi hicho cha mpito, wateja wa Twiga Bancorp wataanza kupatiwa huduma katika matawi ya benki ya posta.

Benki kuu ya Tanzania iliamua kuunganisha taasisi hizo mbili za kifedha baada ya benki ya Twiga Bancorp kushindwa kujiendesha kutokana na mtaji wake kushuka hivyo kuhatarisha amana ya wateja wao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter