Home VIWANDAUZALISHAJI NSSF, Bakhresa kushirikiana uzalishaji sukari

NSSF, Bakhresa kushirikiana uzalishaji sukari

0 comment 177 views

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Bakhresa wapeana ujuzi kuhusu kuwekeza katika kilimo cha miwa na viwanda vya sukari ili kukidhi mahitaji ya bidhaa hiyo hapa nchini. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio amesema kuwa baada ya kutembelea shamba la miwa la Bakhresa lililopo Bagamoyo mkoani Pwani, ameona kuna umuhimu wa kushirikiana na kampuni hiyo ili kukidhi mahitaji ya sukari nchini.

Imeelezwa kuwa kwa mwaka, sukari inayohitajika nchini ni tani 670,000 lakini sukari inayozalishwa ni tani 320,000 pekee. Licha ya kwamba uzalishaji wa sukari umeongezeka kutoka tani 293,075 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi tani 303.431.14 mwaka 2017/18.

Mkurugenzi huyo amemshukuru Bakhresa kwa ushirikiano wake na mawazo mazuri kuhusu uwekezaji wa sukari, na kueleza kuwa wamejifunza mambo mengi kupitia ziara waliyoifanya kwenye shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 10,000 ikiwa ni pamoja na tafiti walizozifanya na jinsi wanavyohifadhi maji shambani hapo.

Kwa upande wake, Bakhresa amesema kuwa wataendelea kufanya mikutano na NSSF ili kupeana ujuzi katika uwekezaji kwenye viwanda vya sukari huku akiongeza kuwa, ujenzi wa kiwanda cha sukari ni njia mojawapo ya kuchochea uwekezaji kwenye sekta hiyo kwa manufaa ya taifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter