Home VIWANDAUZALISHAJI Serikali ya Tanzania kujenga uchumi jumuishi

Serikali ya Tanzania kujenga uchumi jumuishi

0 comment 113 views

Serikali inalenga kujenga uchumi jumuishi unaokua kwa kasi na unaoimarisha ustawi wa watu kwa kuboresha huduma za jamii na kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Ameeleza kuwa ili kuwezesha hilo kwanza ni amani na utulivu kwenye nchi pili ni mifumo ya haki inayoeleweka na tatu ni mifumo mizuri ya kodi.

“Mkusanyiko wetu leo hapa ni kuliangazia hili swala la kodi, kama mnavyojua jambo ambalo ni gumu sana kueleweka duniani ni hili la kodi, kodi ni swala gumu hakuna anaelipenda, haswa inayotokana na mapato yako.

Unawasikia wafanyakazi kila siku tupunguziwe kodi ni kubwa, lakini wafanyabiashara na wenyewe malalamiko, wengine malalamiko, kwa hiyo jambo la kodi halijawahi kuwa rahisi,” ameeleza Rais Samia.

Amesema kuwa kwa kufuatia mashauriano na wadau mbalimbali serekali imeendelea kulifanyaia kazi swala la kodi nchini pamoja na mambo mengine waliofanya wameimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato na kuijengea uwezo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Nyingine ni kuimarisha mazingira ya kufanya biashara nchini ikiwemo kwa kufuta baadhi ya tozo na kuimarisha utendaji kwenye idara za serikali, wakala na taasisi mbalimbali.

“Hata hivyo kwa mujibu wa TRA, mwaka 2023/2024 mapato ya kodi yamefikia takribani asilimia 12 ya pato la taifa, kwa hiyo bado tupo chini, tuna kazi ya kufanya,” ameeleza Rais.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter