Home VIWANDAUZALISHAJI Tanzania, Misri kuendeleza ushirikiano miradi ya umeme

Tanzania, Misri kuendeleza ushirikiano miradi ya umeme

0 comments 59 views

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, amesema Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano  kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme na kudunisha ushirikiano uliowekwa na waasisi wa nchi hizo.

Kapinga ameyasema hayo Machi, 2025, mkoani Pwani wakati alipofanya ziara katika mradi wa umeme wa  Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty  ikiwa ni sehemu ya ziara ya  kikazi ya Waziri Badir na ujumbe wake.

“Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa msingi imara wa utekelezaji wa miradi huu wa  umeme na tumeona  matunda halisi ya usimamizi wake,’’ amsema Mhe.Kapinga

Amesema nchi ya Misri imetekeleza mradi huo wa JNHPP  kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya Tanzania ambapo mpaka sasa mashine nane kati ya tisa zimewashwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa JNHPP, Waziri, Dkt Badir Abdelatty, amesifu ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuishukuru Tanzania kwa  kuiamini nchi yake kutekeleza mradi huo wa JNHPP, kwani utawanufaisha wananchi wa Tanzania walio wengi hususani wale wanaozungukwa na eneo la mradi.

Amesema nchi za Afrika zinapaswa kujivunia uwepo wa miradi ya umeme kwa maendeleo ya Waafrika wenyewe na kuahidi kuwa Misri itaendeleza ushirikiano na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi mingine kama hiyo.

Kwa upande wake  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Dannis Londo amesema Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ulionao ili kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi hususani kwenye miradi ya sekta ya Nishati.

Ziara hiyo imehudhuriwa na  Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi wa Misri nchini Tanzania, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta,  Dk James Mataragio, na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Wizara  ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!