Home KILIMOKILIMO BIASHARA Tutaendelea kuunga mkono wawekezaji kwenye kilimo: Bashe

Tutaendelea kuunga mkono wawekezaji kwenye kilimo: Bashe

0 comment 189 views

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali itaendelea kuunga mkono wawekezaji wanaoonesha nia ya kuwekeza kwenye uongezaji thamani wa zao la alizeti hususan katika kuzalisha mafuta ya kupikia.

Amesema hayo alipokutana kwa mazungumzo na wawakilishi kutoka Kampuni ya Mainland Group kutoka ya China Juni 24, 2024 jijini Dodoma.

“Zao la alizeti ni miongoni mwa mazao ya kimkakati, hivyo Serikali itaendelea kusimamia miongozo zikiwemo sheria ili kuwalinda wawekezaji wanaowekeza kwenye uzalishaji wa mafuta ya alizeti,” ameeleza Waziri Bashe.

Kwa upande wake, Meya wa jimbo la Hunan nchini China, Xiewei Fieng ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuikaribisha kampuni ya Main Land Group kuwekeza nchini katika kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti katika eneo la Veyula, mkoani Dodoma.

Aidha, Waziri Bashe ameipongeza kampuni ya Mainland Group kwa kujenga kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti na kuwahikishia kuwa upatikanaji wa malighafi utakuwa wa uhakika kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa mbegu za ruzuku za alizeti kwa wakulima nchini ili wazalishe kwa wingi na kukidhi mahitaji ya viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter