Home VIWANDAUZALISHAJI Uchafu wa mazingira unavyorudisha nyuma uzalishaji

Uchafu wa mazingira unavyorudisha nyuma uzalishaji

0 comment 78 views

Serikali mbalimbali duniani zinajaribu kuchukua hatua kadhaa katika kupambana na athari za uharibifu na uchafuzi wa mazingira. Hii inatokana na ukweli kwamba shughuli zozote zinazofanywa kwa weledi mkubwa lazima zizingatie uwepo wa mazingira mazuri, safi, rafiki, na salama. Uchafuzi wa mazingira umekuwa ukiathiri shughuli za uzalishaji kwa kiasi kikubwa sana duniani kote.

Zipo aina mbalimbali zinazohusisha moja kwa moja uchafuzi wa mazingira na uharibifu ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa maji, uchafuzi wa ardhi na udongo.

NEMC ni Baraza la Usimamizi wa Mazingira nchini Tanzania lililoanzishwa mwaka 1983 likijishughulisha na:

  • Kuimarisha na kuhakikisha kufuata viwango vya kitaifa vya ubora wa mazingira.
  • Kuchunguza Taarifa ya Madhara na kufanya ufuatiliaji wa mazingira na ukaguzi wa miradi na vifaa.
  • Kufanya na kuratibu utafiti, na uchunguzi katika uwanja wa mazingira na kukusanya, na kusambaza taarifa.
  • Kufanya utafiti na tafiti kwa usimamizi sahihi na uhifadhi wa mazingira.
  • Kutoa ushauri na msaada wa kiufundi kwa vyombo vinavyohusika na maliasili na usimamizi wa mazingira.
  • Kuanzisha na kubadili taratibu na ulinzi wa kuzuia ajali ambazo zinaweza kusababisha uharibifu wa mazingira.
  • Kuimarisha elimu ya mazingira na ufahamu wa umma; na kuanzisha pamoja na kuendesha mfumo wa kitaifa wa habari wa mazingira kwa ajili ya usimamizi wa mazingira bora.

Licha ya NEMC kuchukua hatua kadhaa katika kuboresha hali ya mazingira nchini ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa matumizi ya nishati mbadala mfano uhimizwaji wa matumizi ya gesi kupikia badala ya kuni na mkaa, matumizi ya samadi na mboji badala ya mbolea ya kisasa, urejelezaji baada ya matumizi, mfano maji jijini Mbeya, bado suala la uchafuzi wa mazingira ni kubwa katika jamii hasa kwenye miji kama Dar es salaam.

Madhara ya uchafu wa mazingira

  1. Ongezeko la joto duniani kutokana na wana sayansi kugundua uharibifu wa safu ya ozoni inayozuia kiasi kikubwa cha joto kwenye anga
  2. Ongezeko la magonjwa ya mlipuko Kama Kipindupindu na kansa ya ngozi. Hivi karibuni imeshuhudiwa ongezeko la watu wenye kansa duniani hali inayotishia usalama wa maisha ya watu wengi kutokana na athari za jua, moshi wa viwandani, na magari.
  3. Upungufu wa mvua. Utafiti uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania Septemba 2015 jijini Dar es salaam na Mtabiri Mwandamizi Wilberforce Kikwasi ulionesha kuwa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na jamii unachangia kwa kiwango kikubwa kusababisha upungufu wa mvua nchini

Uzalishaji unaathirika vipi?

  1. Uharibifu wa miundombinu. Uchafuzi wa mazingira umekuwa ukichangia uharibifu wa miundombinu ikiwa ni pamoja na miundo mbinu ya maji, barabara na Reli hali inayorudisha maendeleo ya taifa kwa kuhitaji ukarabati upya
  2. Ongezeko la magonjwa linalosababisha kupungua kwa nguvu kazi nchini kutokana na magonjwa na vifo
  3. Matumizi ya pesa katika kuboresha mazingira yaliyoharibiwa inahitaji pesa yingi na muda wa kutosha na kuna mazingira ambayo kwa namna moja au nyingine hauwezi kuyaboresha tena yakishaharibiwa.

Nini kifanyike?

  1. NEMC na wadau wengine wa mazingira bado wana kazi kubwa kuhakikisha kuwa elimu inazidi kutolewa mijini na vijijini juu ya njia bora za utunzaji mazingira. Hali itakatyo wafanya wananchi kuamka na kujua umuhimu wa utunzaji mazingira
  2. Serikali, sekta binafsi, na mashirika wanao wajibu wa kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kama njia pekee itakyo saidia kuondoa tatizo hili. Mfano kuhamasisha matumizi ya gesi kupikia badala ya mkaa, Mkakati ambao tumeona serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiutilia mkazo kwa kuanzisha sera ya “ Mkaa gharama tumia nishati mbadala.”
  3. Elimu ya utunzaji mazingira isisitizwe au ikiwezekana iwe kwenye mtaala toka awali ili kuwajengea watoto uwezo wa kujua mapema athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira.
  4. Utoaji wa tuzo kwa watunzaji wa mazingira sambamba na adhabu kwa wachafuzi wa mazingira. Tumeshuhudia sehemu mbalimbali nchini hasa katika miji mikubwa watu wakikamatwa na kuwajibishwa katika vyombo vya dola kutokana na uchafuzi wa mazingira, lakini pia kuna maeneo watu wamepewa tuzo kwa kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa vitendo hali inayoleta motisha kwa watu wengi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter