Home VIWANDAUZALISHAJI Uingereza yavutiwa na mkakati wa Tanzania kuongeza thamani madini nchini

Uingereza yavutiwa na mkakati wa Tanzania kuongeza thamani madini nchini

0 comment 10 views

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Lord Collins amevutiwa na mpango wa nchi ya Tanzania kuandaa mkakati maalum wa uongezaji thamani madini nchini Tanzania na kuahidi kwamba Uingereza itatoa ushirikiano katika kusaidia eneo la uongezaji thamani madini hayo ndani ya nchi.

Hayo yamesemwa wakati wa kikao kati ya Lord Collins na Waziri wa Madini Anthony Mavunde kilichofanyika Jijini Dar es salaam.

“Tanzania na Uingereza zina ushirikiano wa muda mrefu katika maeneo mengi ya kiuchumi ikiwemo sekta ya Madini.

Nimevutiwa na mkakati wa Tanzania wa kuongeza thamani ndani ya nchi, mkakati ambao Uingereza tunauunga mkono na tupo tayari kuwezesha utekelezaji wake kupitia Mradi wa “Manufacturing Africa“ ambapo pauni 2.1 bilioni zimetengwa kusaidia nchi 6 za Afrika, ikiwemo Tanzania, kutengeneza bidhaa za kati na za mwisho kupitia madini,” alisema Lord Collins.

Akizungumza katika Kikao hicho,Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema Tanzania inayo mkakati wake maalum wa uongezwaji thamani madini ili kuongeza manufaa makubwa zaidi kwa nchi kupitia sekta ya madini ambapo kwa sasa madini yanapaswa kuchakatwa na kuongezwa thamani nchini.

Serikali imetenga eneo maalum la ujenzi wa viwanda vyakuongeza thamani Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga kwa lengo la kuvutia uwekezaji katika eneo hili.

“Mradi wa “Manufacturing Africa“ utasaidia kufanikisha azma ya Tanzania kwa kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vya kuchakata, kusafisha na kutengeneza bidhaa zitokanazo na madini,“ alisema Mavunde.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza  Mbelwa Kairuki na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Marianne Young.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter