Wanawake hapa nchini wametakiwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha kwa lengo la kujikwamua kiuchumi. Wito huo umetolewa na Meneja wa kikundi cha ujasiriamali cha Msalato jijini Dodoma, Hamida Msofe wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Msofe ameeleza kuwa endapo wanawake wataitikia wito wa kujiunga katika vikundi, itawawezesha kupata mikopo ambayo itatumika kujiajiri na kuongeza kipato chao. Meneja huyo amesema hatua hiyo itasaidia wanawake kutokuwa tegemezi kwani watakuwa na miradi yao wenyewe.
Pamoja na hayo, ameshauri vikundi vya wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kujiweka katika nafasi nzuri katika soko la ndani na hata la njehuku akiwasisitiz kuwa, ubora wa bidhaa unaweza kuwainua zaidi kiuchumi.
“Changamoto iliyopo kwenye vikundi ni utengenezaji wa bidhaa ikiwamo vifungashio vya bidhaa kukosa ubora na kusababishwa kushindwa katika ushindani wa soko la bidhaa mbalimbali”. Amesema Msofe.