Home KILIMO Kilimo Smart: Kilimo bora mkononi

Kilimo Smart: Kilimo bora mkononi

0 comment 173 views

Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ni wakulima hivyo kilimo ni sekta muhimu sana hapa nchini. Serikali na sekta binafsi zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali na kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo chao. Ili kuendeleza kilimo bora kuna kila sababu ya kujihusisha zaidi na programu mbalimbali ambazo zimekuwa zikigunduliwa ili kurahisisha kilimo.

Kilimo Smart ni programu ambayo ilianzishwa Agosti 2018, na wanafunzi watano kutoka vyuo vya Sokoine, Chuo cha Kikatoliki cha Nairobi, Chuo cha Mzumbe, Chuo cha Mati Mlingano na Chuo cha Sunway kilichopo Malaysia. Programu hii ni muhimu kwa kila mkulima kuitumia kwani  kuna uhakika wa kujifunza mambo mapya kuhusu kilimo biashara, ufugaji wa kisasa, magonjwa ya mazao, kupata ushauri wa udongo na vilevile kufanya manunuzi.

Kupitia programu hii mkulima ana uwezo wa kufikia machapisho yaliyopo hata akiwa hajajiunga na mtandao wa intaneti. Hivyo kwa urahisi zaidi mtumiaji anaweza kupata machapisho mbalimbali na kusoma bila kutumia data.

Mbali na kuelimisha wakulima, timu ya Kilimo Smart pia imelenga kutoa elimu kwa vitendo kupitia shamba darasa, ili kutoa nafasi kwa wakulima kujifunza kwa vitendo ili kuelewa zaidi na kuongeza ufanisi katika kilimo wanachofanya. Aidha, inaelezwa kuwa waanzilishi hao wana malengo ya kuuza pembejeo kwa bei rafiki ili kuwaunga mkono wakulima hapa nchini.

Kumekuwa na malalamiko ya masoko kwa muda mrefu. Katika kutatua changamoto hiyo, kuna umuhimu mkubwa wa kutumia programu kama hizi kwani ni rahisi kuwafikia watu wengi zaidi kwa wakati mmoja na kupata wateja kwa wingi. Programu hii inapatikana Playstore kwa watumiaji wa simu zenye mfumo wa Android.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter