Home VIWANDAUZALISHAJI Wadau wa mchele walilia masoko

Wadau wa mchele walilia masoko

0 comment 49 views

Wakulima wa mpunga hapa nchini wameiomba serikali kufuta zuio la usafirishaji wa mchele nje ya nchi kutokana na ziada iliyopo hivi sasa ya tani 1.2 milioni kukosa soko la uhakika ndani ya nchi. Wakulima hao wamedai sintofahamu inayoendelea sokoni imepelekea kudorora kwa bei ya mchele, hivyo kuwasababishia hasara kwani gharama ya uzalishaji ni kubwa. Mbali na wakulima hao kuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusikiliza kilio chao, pia wamedai serikali imekuwa ikiwahamasisha kuzalisha kwa wingi lakini imeshindwa kuwapatia masoko ya uhakika, hali ambayo inapelekea idadi kubwa ya wakulima hao kukata tamaa.

“Serikali inatushauri tuzalishe mpunga kwa wingi, lakini cha kushangaza masoko hakuna, tunaiomba itupatie kibali cha kuuza bidhaa zetu nje ya nchi ili tuweze kupata faida ya kilimo tunachofanya”. Ameeleza mmoja ya wakulima wa zao hilo.

Septemba 12 mwaka huu, serikali ilitangaza kusitisha uagizwaji wa mchele kutoka nje ya nchi kwa madai kuwa uliopo nchini unajitosheleza, huku ikielezwa kuwa, tani 2.2 za mchele zilizopo hapa nchini ni matokeo ya wakulima wa mpunga kupatiwa mbinu bora na za kisasa. Akitolea ufafanuzi suala hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mathew Mtigumwe alisema mahitaji ya nchi kwa sasa ni tani 900,000 hivyo uzalishaji umeongezeka na kuna ziada ya tani 1.2 milioni.

Wakati hayo yakiendelea hapa nchini, nchi jirani ya Kenya imezuia uingizaji wa mchele kutoka Tanzania, dalili inayoashiria mvutano wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili. Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolph Mkenda amesema kilichopelekea zuio hilo ni ubora wa mchele pamoja na jinsi unavyofungashwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter