Home VIWANDAMIUNDOMBINU JPM aomba Japan kujenga miundombinu Dodoma

JPM aomba Japan kujenga miundombinu Dodoma

0 comment 112 views
Na Mwandishi wetu

Baada ya kukutana na Rais wa Shirika la Kimaendeleo la Japan (JICA) Dk.Shinichi Kitaoka, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameomba shirika hilo kufadhili na kuboresha miundombinu katika makao makuu ya nchi Dodoma katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Rais Magufuli amesema Tanzania inathamini mchango mkubwa wa JICA katika miradi mbalimbali ya maendeleo kote nchini na kuomba shirika hilo kuangalia uwezekano wa kujenga miundombinu Dodoma, ambako serikali imedhamiria kuhamia kama ishara ya urafiki na mahusiano mema baina ya Tanzania na Japan.

Naye Rais wa JICA, Dk. Kitaoka ambaye amewasili hapa nchini kwa mara ya kwanza ametoa pongezi zake kwa Rais Magufuli kwa uongozi mzuri, mapambano yake dhidi ya rushwa na jitihada zake katika kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Amesema jitihada zake zote zinasaidia kuinua uchumi. Ameahidi JICA itaendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter