Na Mwandishi wetu
Baada ya kutembelea miradi ya umeme wa gesi ya Kinyerezi I na Kinyerezi II wilayani Ilala jijini Dar es salaam, Kamati ya Bunge la Bajeti imesema kuna sababu ya kufanya mabadiliko kwenye Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa taasisi za serikali.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Ghasia amesema baada ya ziara yao, Meneja mradi wa Kinyerezi Stephen Manda alieleza kamati hiyo kuwa kodi ya VAT inachelewesha utekelezwaji wa miradi mbalimbali katika shirika hilo.
Manda amedai kuwa vifaa vimekua vikikwama bandarini sababu ya kodi hivyo sheria hiyo inapaswa kuangalia upya kwa taasisi za serikali kwani lengo kubwa ni kuleta maendeleo ya taifa letu.
Ghasia pia mbali na hayo, ameelekeza uongozi wa Shirika la Mafuta ya Petroli Tanzania (TPDC) kuweka maandalizi ya miundombinu ya gesi katika maeneo ambayo viwanda vitajengwa. Kufanya hivyo kutasaidia wawekezaji