Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wanawake wafanye haya kulinda biashara zao

Wanawake wafanye haya kulinda biashara zao

0 comment 130 views

Tovuti ya Medium.com imeeleza kuwa 54.3% ya biashara ndogo na za kati (SMEs) nchini zinamilikiwa na kuendeshwa na wanawake, ambao wengi wao wana umri kati ya miaka 25 na 40 huku wakiwa na elimu ndogo. Hivyo basi mbali na serikali pamoja na taasisi zisizokuwa za kiserikali kuendelea kutoa misaada na elimu kwa wajasiriamali nchini ili waweze kunufaika na biashara zao na kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini. Katika upande wa wanawake kuna baadhi ya mambo ambayo wanaweza kuyafanya  ili waweze kulinda biashara zao hii itawasaidia kuwekeza nguvu zaidi katika uzalishaji na kutafuta masoko.

Mambo hayo ni kama yafuatayo:

Kutofautisha masuala ya biashara na masuala binafsi

Ieleweke kuwa wafanyabiashara wengi waliofanikiwa wamekuwa wakitofautisha masuala binafsi na ya kibiashara. Kutokana na majukumu ambayo wanawake huwa nayo majumbani na hata katika sehemu za biashara kuna muda huwa wanajikuta wakichanganya pande hizo mbili bila kujua athari ambazo zinaweza kutokea hapo mbeleni ikiwa upande mmoja utapata changamoto. Hivyo basi ili kujiepusha na athari zozote katika pande hizo mbili inashauriwa kutenganisha mambo binafsi na yanayohusu biashara hususani katika suala zima la fedha. Ndio maana katika biashara huwa mmiliki wa biashara anashauriwa ‘kujilipa’ ili kuweza kujikimu kimaisha bila kuharibu mtiririko wa fedha katika biashara.

Kujifunza zaidi masuala ya sheria (Elimu na Ushauri)

Inaelezwa kuwa idadi kubwa ya wajasiriamali hasa wanawake hawana uelewa wa masuala ya kisheria katika upande wa biashara hii imewapelekea wengi wao kushindwa kwa namna moja au nyingine kuendeleza biashara zao kuelekea hatua za mbele zaidi. Hivyo ili kuwa katika upande sahihi na kuweza kuendeleza biashara kwa umakini(kwamfano katika masuala ya mikataba na mikopo) inashauriwa kutafuta njia ambazo zitakusaidia kujua haki zako kama mfanyabiashara na kuweza kupata ushauri kuhusu maamuzi mbalimbali ya kibiashara. Kwamfano siku hizi kuna programu (Application)inayotoa ushauri, elimu na huduma za kisheria nchini, App hiyo inaitwa “Sheriakiganjani” inapatikana  Playstore. Hivyo kama mjasiriamali makini unaweza kupitia tovuti yao https://www.sheriakiganjani.co.tz/ ili kuweza kuona huduma  wanazotoa na hata kuuliza maswali zaidi ili kuweza kupata ujuzi zaidi na msaada stahiki kuhusu masuala ya kisheria katika upande wa biashara.

Kuimarisha Ushiriki katika vyama vya wajasiriamali wakike

Kwanza ni muhimu kwa wanawake nchini kujua taasisi mbalimbali za masuala ya ujasiriamali na vigezo na masharti ya kujiunga na taasisi hizo ili kuweza kunufaika, na kukua kupitia taasisi hizo. Pia vyama  mbalimbali nchini, vinahitaji kuratibiwa ili waweze kuunda mtandao, na hivyo kuwezesha ugawanaji wa habari, huduma, mafunzo, na rasilimali, ambazo zinaweza kuboresha ushirika wa vyama hivyo. Hii itasaidia vyama vyenye  nguvu kuleta kuongeza ufanisi na kuleta mabadiliko kikanda na kitaifa pia. Mbali na wanawake wajasiriamali nchini kuendelea kujihusisha na Taasisi ya kiserikali inayojihusisha na maendeleo ya viwanda vidogo nchini (SIDO), kuna umuhimu kwa wanawake kujiunga na taasisi nyingine za kiserikali na zisizo za kiserikali au kuunda makundi yao ili kuweza kunufaika zaidi.

Pata leseni zinazohitajika katika biashara

Leseni ya biashara humuhakikishia mfanyabiashara kuwa anaweza kuendesha biashara yake kihalali, mara tu baada ya kusajili. Pia kuwa na leseni husaidia ufuatiliaji wa masuala ya ushuru. Pia huhakikisha biashara hiyo inakidhi mahitaji ya chini ya kulinda afya ya umma na inaarifu raia kuhusu shughuli ambazo zinaweza kuathiri umma.

Ieleweke kuwa kila biashara huhitaji leseni na vibali maalum kulingana na tasnia husika. hivyo ni vyema kufika katika taasisi husika inayojihusisha na masuala ya leseni na vibali ili kuweza kupata vibali vyote vinavyohitajika ili kuepukana na masuala ya kisheria mbeleni ikiwa ni pamoja na kufunga biashara kutokana na ukosefu wa vibali.

Mbali na hayo, wajasiriamali wengi hususani wanawake wamekuwa wakikata tamaa ya kuanzisha biashara zao au kuziendeleza katika hatua kubwa zaidi kutokana na vigezo na masharti magumu kutoka katika taasisi mbalimbali pamoja na mlolongo mrefu ambao hutumia muda mrefu. Hivyo kuna umuhimu kwa Taasisi husika kutengeneza michakato rahisi kwa wafanyabiashara ili waweze kuanzisha na kuendeleza biashara zao bila kupoteza muda mwingi katika masuala ya kisheria, kujisajiri, kubadilisha leseni zao nk.

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter