Home KILIMOKILIMO BIASHARA LIFAHAMU ZAO LA PAMBA

LIFAHAMU ZAO LA PAMBA

0 comment 120 views

Hapa nchini, zao la pamba hulimwa zaidi na wakulima wadogo katika mikoa mingi ikiwemo Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora, Mara, Kagera, Singida, Kigoma na Katavi. Mikoa ya Shinyanga na Mwanza inaongoza kwa kulima zao hili kwa wingi zaidi. Mbali na hayo, kuna mengi ambayo watu hawafahamu kuhusu zao hili.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na haya yafuatayo:

ADVERTISEMENT

– Neno ‘pamba’ limetokana na neno la kiarabu ‘Kutun’ au ‘Qutun’ ambalo linamaanishha kitambaa chochote kilaini; ndio maana vitambaa vya kusokotwa vilivyokuwa vikitengenezwa kwa nyuzi laini zilizokuwa zikitengenezwa kutokana na mmea wa pamba zilitokea katika ulimwengu wa kiislamu.

– Mbali na pamba kutumika kutengenezea nguo pia hutumika kutengenezea mipira, vifaa vya matibabu, fedha za karatasi, mafuta ya kula nk.

– Kuna aina zaidi ya 43 za pamba duniani, ambapo baadhi kati ya hizo hukua katika miti. Pia ni aina nne za pamba hulimwa kwa ajili ya biashara.

– Mmea wa pamba huhitaji takribani siku 180-200 tangu pale unapopandwa kukua na kuwa tayari kwa ajili ya mavuno.

– Huko Amerika Kusini pamba huja katika rangi mbalimbali ikiwa ni pamoja na rangi nyekundu, njano, zambarau, kijani, na nyuzi za rangi ya chuichui.

– Fedha ya karatasi ya nchini Marekani ina mchanganyiko wa 75% ya pamba na 25% ya katani.

– Hadi sasa bei elekezi ya pamba hapa nchini ni Sh. 1,200 kwa kilo. Serikali imekuwa ikiwasisitiza wakulima kuunda vikundi ili kuweza kunufaika zaidi na zao hilo ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vitakavyotumika kutengeneza nguo na nyuzi nchini badala ya kuuza zao hilo nje ya nchi.

– Zao la pamba ni zao la pili kubwa kuuza nje ya nchi baada ya zao la kahawa. Pia kwa upande wa Afrika ni zao la nne kufanya mauzo nje ukiachana na mataifa matatu ya mwanzo ambayo ni Mali, Burkina Faso na Egypt.

Serikali ina mpango wa kuwekeza zaidi katika zao hilo ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya kuchakata zao hilo ili kuweza kuwanufaisha wakulima kiuchumi na kuleta maendeleo zaidi kuelekea uchumi wa kati.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter