Home BIASHARA UMUHIMU WA TEKNOLOJIA YA KOMPYUTA KATIKA BIASHARA

UMUHIMU WA TEKNOLOJIA YA KOMPYUTA KATIKA BIASHARA

0 comment 247 views

Uvumbuzi wa kompyuta umebadilisha tasnia nyingi duniani, Biashara na kampuni nyingi hivi sasa wanatumia kompyuta ili kurahishisha kazi. Kupitia programu sahihi ambazo hutumika katika kompyuta kampuni nyingi zimejipatia mafanikio makubwa kwa muda mfupi. Kila ofisi siku hizi hutumia kompyuta ili kurahisisha ufanisi wa kazi. Kwa wafanyabiashara wasiotumia kompyuta katika ofisi zao wakati wa kwenda na kasi ya teknolojia umewadia.

Zifuatazo ni faida za kutumia kompyuta kwa wafanyabiashara:

Mawasiliano: Mawasiliano ya ndani na nje hufanyika kwa urahisi na haraka kupitia mfumo wa barua pepe unaopatikana kwenye kompyuta. Wafanyakazi wanaweza kuwasiliana haraka zaidi kupitia kompyuta. Pia ikitokea watu wako mbali na wanahitaji kuwasiliana wanaweza kutumia kompyuta kufanya hivyo kwa kutumia programu mbalimbali za video kama Skype na nyingine nyingi.

Kuhifadhi na kuzifikia taarifa: Kupitia kompyuta mtumiaji hupata urahisi wa kuhifadhi taarifa na kumbukumbu na pindi anavyokuwa anazihitaji huwa ni rahisi kwa mhusika kuzifikia habari husika ikilinganishwa na utunzaji wa nyaraka katika makaratasi/mafaili jambo linaweza kuchukua muda kwa kampuni zenye nyaraka nyingi. Lakini kwa kompyuta utafutaji wa nyaraka hufanyika dakika chache hivyo kuepusha upotevu wa muda.

Kutengeneza mtandao (intranet): Ni rahisi kwa wafanyakazi kushirikiana kuhusu masuala ya kazi kupitia kompyuta kwa urahisi zaidi. Hii inatumika pia kwa programu na usimamizi wa kompyuta, ambazo hupunguza gharama za ofisi, kwani wanaweza kununua bidhaa moja ya programu inayoweza kusambazwa badala ya kununua nakala nyingi kwa kila mtu.

Uzalishaji: Inaelezwa kuwa matumizi ya kompyuta husaidia mambo mengine mbali na kutuma ujumbe, usimamiaji wa data, upokeaji wa habari.

ADVERTISEMENT

Aidha, kila jambo lenye faida huwa na hasara zake hivyo ni muhimu kwa watumiaji kutumia kompyuta kwa kiasi ili kuepuka changamoto mbalimbali. Pia matumizi ya muda mrefu ya kompyuta humaanisha muda mrefu wa kukaa jambo ambalo linaweza kuleta athari kIafya.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter