Home BIASHARA Benki ya NMB kuvutia watalii kutoka barani Asia kupitia UnionPay

Benki ya NMB kuvutia watalii kutoka barani Asia kupitia UnionPay

0 comment 125 views

Katika kuwavutia watalii kutoka barani Asia na kwingineko duniani, benki ya NMB imeshirikiana na kampuni ya kimataifa ya kadi –Union Pay International (UPI) ili kuwawezesha watumiaji wa kadi za UnionPay kufanya miamala kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) na PoS za benki hiyo.

NMB pia imezindua jukwaa la biashara ya mtandaoni ‘E- Commence platform’  litakalowezesha wafanyabiashara kufanya miamala kupitia tovuti zao.

‘E Commence platform’ itawawezesha wafanya biashara na makampuni ya huduma kupokea malipo kimtandao kupitia tovuti zao, bila wateja kutembelea sehemu za biashara zao.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema ushirikiano na UPI utaleta unafuu na uharaka wa kufanya miamala kwa watumiaji wa kadi za UPI watakao kuwa wanapata huduma kwenye  ATM na PoS za NMB muda wote.

Zaipuna amesema “hii ni hatua muhimu sana katika kuleta huduma bora kwa wateja wetu, ni fursa kwa wafanya biashara hususani sekta ya utalii, hoteli, na maduka katika kuwezesha biashara za kimataifa kupitia malipo mtandao yanayowezeshwa na benki ya NMB,”.

Amefafanua kuwa  “Kwa mtandao wetu wa zaidi ya PoS 1,750 na ATM Zaidi ya 800 nchini, huduma hii inategemewa kuleta mapinduzi kwa watumiaji wa kadi za UnionPay.

Kadi hizi  zinajulikana kama nyenzo muhimu ya malipo kwa kufanikisha biashara, utalii na muingiliano wa kiutamaduni kati ya bara la Afrika na Asia. Ushirikiano huu kati ya benki ya NMB na UnionPay International utaongeza matumizi ya kadi za UnionPay nchini na katika miamala ya kimataifa na inaashiria mapinduzi ya teknolojia ya malipo kupitia kadi”

Meneja Mkuu wa UnionPay International tawi la Afrika – Luping Zhang amesema wanayo furaha kushirikiana na benki ya NMB kuleta huduma hii muhimu kwa sekta ya utalii Tanzania.

Hang amesema UPI ina takribani kadi bilioni 8.4 zilizopo katika nchi 61 duniani na inajivunia kuwa kampuni kubwa zaidi ya kadi duniani.

Kadi hizi za Union Pay zitasaidia kuongeza wigo wa mauzo na malipo ya watalii nchini, kwani kabla ya hapo malipo mengi yalifanyika nje ya nchi na hivyo kulikosesha taifa mapato yatokanayo na biashara ya utalii.

Kwa bara la Afrika, ipo katika nchi 50.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter