Home BIASHARA Kigamboni yatenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo

Kigamboni yatenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo

0 comment 180 views

Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam imetenga ekari nne kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri amesema “pale ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi tuna ekari nne, tumetenga kwa ajili ya wajasiriamali wadogo mama lishe, baba lishe wamachinga na biashara ndogo ndogo zote. Pale kuna fursa kubwa, pembeni tunajenga stendi na kuna hospitali ya Wilaya pale hivyo mnaweza mkafanya biashara mbalimbali”.

Ameeleza kuwa maeneo hayo hayauzwi hivyo wananchi wachangamkie fursa hiyo.

“Wewe tuambie unataka eneo kiasi gani na unafanya biashara gani tutakukatia eneo lile na masharti ya kujenga vibanda ili muweze kufanya biashara, na tutaendelea kutenga maeneo mengine makubwa zaidi ili wafanya biashara wetu waweze kufanya biashara katika mazingira rafiki,” amesema Msafiri.

Ametoa wito kwa kina mama na vijana wajasiriamali kuchangamkia fursa zilizopo kujikomboa kwenye umaskini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter