Home BIASHARAUWEKEZAJI Acacia yakuza uchumi wa Tanzania

Acacia yakuza uchumi wa Tanzania

0 comment 38 views

Utafiti wa Ernst and Young (EY) waonyesha mchango endelevu wa Acacia kwa Uchumi wa Tanzania

 

  • Dola za Kimarekani 434 milioni (TZS984 bilioni) zilinunuliwa kutoka kwa watoa huduma ndani ya Tanzania.
  • Mchango wa jumla wa Dola za Kimarekani 712 milioni(TZS1.61 trilioni) kwa uchumi wa nchi.

 

Ripoti huru iliyotolewa hivi karibuni na Ernst and Young (EY) inaonyesha mchango mkubwa ambao migodi mitatu ya Acacia – North Mara, Bulyanhulu na Buzawgi – inaendelea kutoa kwa uchumi wa Tanzania pamoja na maendeleo mapana ya jamii.

 

Ripoti hiyo iliyopewa jina laMchango kamili wa Kampuni ya Acacia Mining plc nchini Tanzania katika nyanja ya kiuchumi na kodi kwa mwaka 2017, inaonyesha kwamba katika mwaka uliopita, biashara za Acacia zilinunua bidhaa na huduma zenye thamani ya Dola za Kimarekani 434 milioni (TZS984 bilioni) kutoka kwa watoa huduma wanaopatikana Tanzania.Hii ni sawa na asilimia 67 ya manunuzi ya kampuni katika mwaka 2017. Katika kiasi hiki, takribani Dola za Kimarekani 120 milioni (TZS 271 bilioni) za bidhaa na huduma zilinunuliwa kutoka kwa biashara zilizopo katika vijiji vinavyo zunguka migodi hii mitatu.

 

Pamoja na kukabiliana na changamoto kadhaa katika mwaka 2017, Acacia ilichangia Dola za Kimarekani 712 milioni (TZS1.61 trilioni) katika uchumi wa taifa, sawa na takribani asilimia 1.5 ya Jumla ya pato la taifa la Tanzania (GDP). Mchango huu ni pungufu ikilinganishwa na mchango wa Dola za Kimarekani 724 milioni (TZS1.64 trilioni) katika mwaka wa awali. Mchango wa 2017 ulijumuisha Dola za Kimarekani 200 milioni (TZS453 bilioni) kupitia biashara, mchango usio wa moja kwa moja  kupitia watoa huduma wa Dola za Kimarekani 304 milioni (TZS689 bilioni) na michango itokanayo ya Dola za Kimarekani 208 milioni (TZS471 bilioni). Wakati huo huo, migodi mitatu ya Acacia ilitoa mchango wa Dola za Kimarekani 186 milioni (TZS421 bilioni) kupitia kodi kwa Hazina ya Tanzania, ikijumuisha Dola za Kimarekani 101 milioni (TZS229 bilioni) iliyofanywa na kampuni, Dola za Kimarekani 42 milioni (TZS95 Bilioni) iliyofanywa na wafanyakazi wake, na Dola za kimarekani 42 milioni (TZS95 bilioni) za ziada, kupitia kodi zisizo za moja kwa moja.

 

“Ripoti hii inaendelea kuonyesha nia tuliyonayo ya kuendesha biashara yetu katika njia inayonufaisha nchi na jamii zinazozunguka migodi yetu,” Asa Mwaipopo, Mkurugenzi Mkuu, Tanzania, alisema. “Inatia hamasa kuona shughuli zetu hazinufaishi jamii zinazotuzunguka tu, bali taifa kwa ujumla tunapoendelea kusaidia juhudi za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kufikia Dira ya Taifa ya 2025.”

 

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Acacia imetoa ajira kwa watu wapatao 2800 nchini Tanzania, zaidi ya asilimia 96 kati yao wakiwa ni Watanzania na wanalipwa mishahara na stahiki zenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani 111 milioni (TZS251 bilioni). Uwepo wa Acacia umepelekea kuwepo kwa ajira zaidi ya 33,500 na takribani Dola za Kimarekani 345 milioni (TZS782 bilioni) katika mapato ya wafanyakazi. Matumizi ya kampuni katika mnyororo wa usambazaji pekee, uliwezesha karibu ajira 19,000 zisizo za moja kwa moja nchini Tanzania.

 

Pamoja na mchango wake katika uchumi, katika mwaka 2017 migodi yote mitatu ya Acacia ilifanya matumizi yanayoonekana katika miradi yake ya uwekezaji katika jamii inayolenga kusaidia ajenda ya maendeleo ya serikali na Dira ya Taifa 2025. Katika mwaka husika, migodi mitatu iliwekeza zaidi ya dola za kimarekani 3.5 milioni (TZS8 bilioni) katika elimu, afya, miundombinu, maji na vyoo bora.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter