Home BIASHARA Wafugaji kuku sasa kupata soko la uhakika kupitia ufugaji wa mkataba

Wafugaji kuku sasa kupata soko la uhakika kupitia ufugaji wa mkataba

0 comment 170 views

Mradi wa ufugaji wa kuku kwa mkataba ulioanzishwa na Platnum Kuku una lengo la kuwainua wafugaji kiuchumi kwa kuwapa soko la uhakika pindi wanapotaka kuuza kuku hao.

Mkurugenzi wa Platnum Kuku, Ally Mbarouk anasema mkataba huo ni baina ya mfugaji na Platnum Kuku ambapo mfugaji atanunua vifaranga na mahitaji mengine ikiwamo chakula kipindi chote cha ufugaji.

Huu ni mradi wenye lengo la kuwainua wafugaji kiuchumi, kwa wao kuwekeza katika biashara ya ufugaji wa kuku.

“Sisi kazi yetu ni kumhakikishia soko la uhakika kwa kuwanunua kuku wako wote bandani wakiwa tayari. Kwa maana hiyo ukishafuga hauna mawazo ya kutafuta soko la kuuza kuku,” ameeleza Mbarouk.

Mbarouk amesema wajasiriamali wengi wamekuwa waoga kuwekeza kwenye ufugaji wa kuku kutokana na kukosekana kwa masoko ya uhakika.

“Tumeona tuje na huu mradi wa ufugaji wa mkataba ili kuwashika mkono wafugaji wanaoanza ufugaji pamoja na wale ambao wameshaanza kufuga. Mbali na kuwauzia vifaranga amabvyo ni bora, pia tunawapa usimamizi na mwongozo wa kitaalam,” amesema.

Ameeleza kuwa mfugaji ataweza kununua vifaranga kuanzia 200 hadi 500 ambapo kwa mfugaji anayeanza itamgharibu takribani mtaji wa laki tisa (900,000).

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter