Home BIASHARA Waziri aitaka benki ya TIB kusaidia wajasiriamali wadogo

Waziri aitaka benki ya TIB kusaidia wajasiriamali wadogo

0 comment 100 views

Benki ya Maendeleo (TIB) imetakiwa kuja na mpango bora wa kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili waweze kukuza mitaji yao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo ametoa wito huo jan jijini Dar es Salaam alipofanya ziara na kuzungumza na watendaji wa benki hiyo.

Prof. Kitila alisema lengo lake ni kutafuta fursa za uwekezaji ndani nan je ya nchi ili kuchangia uchumi wa taifa.

Alisema “tuna fedha nyingi nje ya sekta zisizo rasmi, huku barabarani kinachoendeea ni kilimo tupu, asilimia 60 ya biashara ni za kilimo au zitokanazo na sekta hiyo. Hii inamaanisha hatuwezi kukuza kilimo bila kuwawezesha watu hawa”.

Alitoa mfano wa soko la mazao ya kilimo la Ubungo kuwa kwa mwaka wanakwenda takribani watu laki saba hadi milioni mbili na kusema ipo biashara kubwa.

Charles Singili ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIB alisema uwekezaji wanaoweza kuwasaidia ni wa miundombinu ya kuwarasimishia maeneo ya biashara.

Aitaja uwekezaji uliofanywa na benki hiyo kwenye miradi mikubwa mpaka kufikia Novemba mwaka huu katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, gesi, umeme, utalii, elimu na usafiri na mawasaliano ni wa jumla ya Sh. bilioni 633.37.

Alibainisha kuwa asilimia 75 ya miradi hiyo ni ya sekta binafsi na 25 ni sekta ya umma ambapo asilimia 80 ni miradi yam da mrefu ya zaidi ya miaka mitano.

Alitaja changamoto za kugharamia miradi ya muda mrefu kuwa ni mtaji mdogo ili kukidhi matakwa ya sheria za benki ya uwekezaji, uchanga wa soko la hisa ambao unapunguza uwezekano wa kuuza hati fungani za muda mrefu, amana nyingi katika mfumo wa benki ni za muda mfupi na uchache wa bidhaa na huduma za kifedha zinazochochea uwekezaji wa muda mrefu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter