Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Mradi wa bomba la mafuta utazalisha ajira: Rais Samia

Mradi wa bomba la mafuta utazalisha ajira: Rais Samia

0 comment 118 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Uganda Roweri Museven wameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga, Tanzania utakaogharimu dola za Marekani bilioni 3.5.

Katika hotuba yake, Rais Samia amesema mradi huo utasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania na kuchochea utafutaji wa mafuta wa pamoja katika eneo la Afrika Mashariki.

“Kati ya kilomita 1,443 za bomba hili kilomita  1,147 zitapita Tanzania ndani ya mikoa nane na wilaya 24 naamini ajira nyingi zitazalishwa hapa, kama mnavyojua tuna deni la kuzalisha ajira zaidi ya milioni saba kwa miaka mitano hii, hivyo mradi huu utaongeza ajira,” amesema.

Amesema mradi huo mbali na kuchochea shughuli za utafutaji pamoja mafuta na gesi kwa eneo la Afrika Mashariki kuna mategemeo ya kupata mafuta kupitia ziwa Eyasi na DRC . “Wenyewe wana mategemeo ya kupata mafuta na miundombinu itakayotumika ni hii ambayo tumekubaliana kujenga,” ameongeza Rais Samia.

Kwa upande wake Rais wa Uganda, Yoweri Museven amewaasa Watanzania na Waganda kutobweteka na mradi huo akitaka fedha zitakazopatikana kutumika kuimarisha sekta nyingine.

“Ninapenda kuwasihi wananchi wa Uganda na Tanzania wasibweteke na kulewa na mafuta na gesi ambazo ni rasilimali zenye ukomo wakasahau sekta nyingine endelevu kama kilimo na biashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter