Home FEDHA Nakwenda kupandisha uchumi: Rais Samia

Nakwenda kupandisha uchumi: Rais Samia

0 comment 230 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaomba Watanzania wampe muda afungue nchi ili aweze kuisimamisha kiuchumi.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu siku 100 tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Sita.

“Nakwenda kuifungua nchi kwa sababu uchumi umeshuka tunatakiwa kupandisha uchumi. Tukifungua nchi, tukiweka mazingira mazuri ya uwekezaji, kazi ambayo tumeifanya vizuri sana.

Nataka niwambie wawekezaji waliosajiliwa kipindi hichi cha March mpaka May ni mara mbili ya waliosajiliwa mwaka jana kipindi kama hiki. Wawekezaji wameanza kuja wengi sana.” amesema Rais Samia.

Amesema lengo la kufungua nchi ni uwekezaji uwe mkubwa, ajira zipatikane, pesa izunguke mifukoni, uchumi wa mtu mmoja mmoja ukue, tuzidi kukusanya mapato na kutanua wigo wa mapato.

“Hilo linataka nchi isimame, iwe na amani na utulivu.” Amesema na kuongeza kuwa hilo ni jukumu la kila Mtanzania.

Rais Samia amesema baada ya kusimamisha nchi kiuchumi watashughulikia mambo mengine ikiwemo katiba na mikutano ya kisiasa ya hadhara.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter