Home BIASHARA Samia ashauri wakulima kuzingatia ubora wa kimataifa

Samia ashauri wakulima kuzingatia ubora wa kimataifa

0 comment 68 views

Makamu wa Rais Samia Suluhu amewaagiza maofisa ugani katika mikoa iliyo pembezoni mwa Ziwa Nyasa kuwaelimisha wakulima ili wazalishe mazao yenye ubora unaofikia mahitaji ya soko la kimataifa zikiwemo nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC).

Samia ametoa agizo hilo wananchi wakati akizungumza na baada ya kufanya ukaguzi katika meli mbili za mizigo sambamba na kukagua maendeleo ya ujenzi wa meli ya abiria ambao bado unaendelea..

Makamu wa Rais ametumia fursa hiyo kuwashauri wakulima katika eneo hilo kuboresha kilimo chao kwani uwepo wa miundombinu ya meli unachochea soko la mazao yanayozalishwa. Vilevile, Makamu huyo ametoa wito kwa wakulima wa ndizi kutoka Kyela na Rungwe kutumia mbinu za kisasa zaidi za kilimo ili soko la kimataifa la zao hilo lianzishwe wilayani Kyela na kuwanufaisha watanzania.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Karim Mattaka amesema ujenzi wa meli za mizigo ulikamilika Julai mwaka jana na meli hizo tayari zinafanya kazi ziwani hapo. Akizungumzia kuhusu ujenzi wa meli ya abiria, Mattaka amedai hadi sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 75 na wanatarajia meli hiyo itakamilika ifikapo mwisho wa mwaka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter