Home BIASHARA Machinga warudi Karume: Rais Samia

Machinga warudi Karume: Rais Samia

0 comment 177 views

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameruhusu wafanyabiashara wa Soko la Karume kurejea na kuendelea na biashara kwa kuwekewa mpango mzuri.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wafanyabiashara hao baada ya kupokea taarifa ya ripoti iliyoundwa kuchunguza chanzo cha moto uliotokea sokoni hapo usiku wa kuamkia January 16, 2022,  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema Rais Samia ameelekeza pia uwepo utaratibu mzuri wa kuzuia majanga.

Amesema hakuna mfanyabiashara atakaedhulumiwa eneo lake na watajenga vibanda kwa gharama zao wenyewe.

Kuhusu ripoti ya chanzo cha moto, RC Makalla amesema kamati imebaini moto huo ulitokana na mshumaa uliowashwa kwenye kibanda walichokuwa wanajihifadhi watumiaji wa dawa za kulevya “mateja”.

Aidha, RC Makalla amesema baada ya kupokea ripoti hiyo ataikabidhi kwenye mamlaka za juu kwa ajili ya utekelezaji wa maoni na mapendekezo yote ya kamati.

Miongoni mwa maoni na mapendekezo ya kamati hiyo ni pamoja ujenzi wa soko jipya linaloendana na hali ya sasa.

Uwepo wa mfumo mzuri wa kuzuia moto, barabara za kuingia na kutoka, ujenzi wa majengo ya muda mfupi, na kila mfanyabiashara kuwa na bima.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Eng. Justin Lukaza amesema hasara iliyotokana na kuungua hilo ni zaidi ya Shilingi bilioni 7.2 na idadi ya wafanyabiashara waliokumbwa na janga hilo ni takribani 3,090.

Wafanyabiashara wamepongeza uamuzi huo na kuishukuru serikali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter