Home BIASHARA TRA yafungia maduka 200 Rukwa

TRA yafungia maduka 200 Rukwa

0 comment 102 views
Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Rukwa imefungia maduka zaidi ya 200 ambayo yameshindwa kutekeleza agizo la kuwa na mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) ndani ya wiki mbili kama ambavyo waliagizwa.

Meneja wa TRA Mkoa wa Rukwa Fredrick Kanyiriri amesema kuwa wafanyabiashara hao walipewa muda wa kutosha kununua mashine hizo lakini wengi hawakufanya hivyo, hali iliyopelekea TRA kufunga biashara zao mpaka watakaponunua EFD na kulipa faini kama sheria inavyoelekeza.

Meneja huyo ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria, wafanyabiashara ambao wanafikisha makusanyo ya Sh. 14 milioni kwa mwaka mmoja wanatakiwa kuwa na EFD ili zitumike kutoa risiti pindi mauzo yanapofanyika.

Kwa upande wao, wafanyabiashara wanadai kuwa gharama ya mashine hizo ipo juu sana jambo ambalo linafanya wengi wao kushindwa kuzimudu hivyo itatakiwa wapewe muda zaidi na mamlaka hiyo ili wajipange. Kwa mujibu wa maofisa wa TRA, mkoa wa Rukwa una wafanyabiashara takribani 308 lakini hadi hivi sasa, ni 108 tu kati yao ndiyo wanatumia mashine za EFD jambo ambalo linakosesha serikali mapato.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter