Daraja la Tanzanite(Salenda) limekamilika kwa asilimia 100 na litaanza kutumika rasmi kesho February Mosi, 2022.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema daraja hilo lenye urefu wa km 1.03 limegharimu kiasi cha Sh bilioni 243.
Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inafunguka kwenye sekta ya miundombinu ili wananchi waweze kufanya kazi zao na nchi iweze kukua kiuchumi kwa asilimia 100.
“Daraja hili ni muhimu sana kwa sababu litapunguza changamoto ya foleni sababu daraja la zamani la Selanda lilikuwa limeshazidiwa na wingi wa magari hivyo kukamilika kwake ni muarobaini kwa foleni za jiji la Dar es Salaam”, amesema Prof. Mbarawa.
“Ufunguzi rasmi wa daraja hili tutaufanya hapo baadae, tutamualika Rais na yeye atafanya ufunguzi rasmi, lakini Jumanne tutawaruhu wananchi waweze kupita waweze kutumia daraja hili,” Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa daraja hilo litaruhusiwa kwa wananchi kulitumia bila malipo kwa saa 24 kwa siku.