Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Parachichi za Kenya kuuzwa China

Parachichi za Kenya kuuzwa China

0 comment 206 views

Baada ya takribani miaka minne ya ushawishi, serikali ya China sasa imeiruhusu Kenya kupeleka zao la parachichi nchini humo.

Mwaka 2019, China ilifungia uingizwaji wa bidhaa hizo baada ya kuenea kwa usafirishwaji wa ndani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kephis Theophilus Mutui amesema “Kenya imepewa fursa ya kupata soko la parachichi nchini China.”

Mwishoni mwa mwezi Januari, Tanzania ilifanikiwa kufungua soko lake la parachichi nchini Afrika Kusini. Soko hilo lililokuwa limefungwa kwa takribani miaka 10.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akisema “kwa wakulima wa Parachichi kwetu Hii ni taarifa njema.

Baada ya miaka mingi Hatimae baada ya Jitihada za Muda mrefu leo Tumefanikiwa kufungua Soko la South Africa

Nitumie nafasi kuwashukuru sana Wataalam wa Wizara ya kilimo na hasa kitengo cha Afya ya MIMEA

Hii ilikua ni kazi ya pamoja nawashukuru sana Sekta Binafsi nawashukuru FAO ambao tulifanya nao hii kazi Soko hili ni muhimu sana kwetu kwa zao la Parachichi hasa swala Msimu wetu na Aina ya Parachichi tunayozalisha”. Tupo hatua za Mwisho kufungua Soko la INDIA.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter