Home AJIRA Tanzania yashiriki mkutano kutatua changamoto soko la ajira

Tanzania yashiriki mkutano kutatua changamoto soko la ajira

0 comment 105 views

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amehutubia Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani, ambapo ameeleza juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu katika kupambana na madhara ya Covid -19 katika soko la ajira.

Katika mkutano huo unaofanyika Geneva, Uswisi Ndalichako amelipongeza Shirika la Kazi Duniani kwa namna lilivyojipanga kusaidia nchi zinazoendelea katika bajeti zijazo na kuonesha utayari wa Tanzania kushirikiana na Shirika hilo katika kutatua changamoto za soko la ajira.

Changamoto hizo ni pamoja na kuzalisha fursa za ajira kwa vijana, kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii, kusimamia viwango vya kazi na kuimarisha uhuru wa majadiliano kati ya waajiri na wafanyakazi.

Miongoni mwa juhudi alizozijata kufanywa na serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto ya soko la ajira ni pamoja na kuanzisha na kutekeleza programu ya taifa ya kukuza ujuzi ambayo imewezesha vijana walio katika mazingira magumu wakiwemo wenye ulemavu kupata fursa ya mafunzo ya ujuzi wa kufanya kazi.

Nyingine ni kusimamia uanzishwaji wa mabaraza ya wafanyakazi, kusimamia kaguzi za kazi sehemu za kazi, kuwezesha Bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa Sekta ya Umma na Binafsi na Maboresho katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter