Home BIASHARA Zanzibar yapewa mafunzo mifumo ya biashara

Zanzibar yapewa mafunzo mifumo ya biashara

0 comment 139 views

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeendesha mafunzo ya mifumo ya biashara kwa maafisa wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.

Mafunzo hayo pia yamejumuisha wadau kutoka sekta mbalimbali za biashara visiwani humo.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Said Shaaban ambaye ni mgeni rasmi katika mafunzo hayo ametoa wito kwa taasisi zote kutumia mifumo ya taarifa za biashara ili kupata taarifa mbalimbali za kuwezesha wafanyabiashara kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TanTrade Dr. Issa Seif ameeleza kuwa elimu iliyotolewa ni muhimu sana kuwawezesha kutumia mfumo mzima wa kufahamu utaratibu wa kupata leseni na vibali vya kuuza bidhaa nje ya nchi, kuingiza bidhaa nchini na kupitisha bidhaa nchini kwenda nchi za nje.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanalenga kuwajengea uwezo viongozi na Maofisa wa Wizara na Taasisi zinazosimamia biashara kufahamu namna ya kutumia mifumo hiyo ambapo itawezesha kuandaa taarifa kutokana na mahitaji ya wafanyabiashara ikiwemo kutoa taarifa za kiintelijensia za biashara pamoja na bei za bidhaa na mazao, upatikanaji wa bidhaa (quantity availability), fursa za uhitaji (opportunities) mahitaji ya masoko (market requirements).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter