Home VIWANDA Malighafi changamoto viwanda Zanzibar

Malighafi changamoto viwanda Zanzibar

0 comment 115 views

Ukosefu wa malighafi umetajwa kuwa moja ya changamoto katika utengenezaji wa bidhaa za nguo kwenye Viwanda vya Idara Maalum (SMZ) Zanzibar.

Viwand hivyo, hulazimika kuagiza vitambaa kwa ajili ya kushona nguo mbalimbali zinazotengenezwa kiwandani hapo nchini China.

Afisa habari wa Viwanda hivyo ambavyo kwa sasa vina jina la MARASHI anasema malighafi hizo ni moja ya changamoto ambapo kwa upande wa utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama viatu wanaagiza ngozi kutoka kwenye viwanda vya Tanzania bara.

“Viwanda hivi vilianzishwa mwaka 2005 kwa ajili ya kutengeneza sare za wapiganaji pekee wa Idara tano Maalum Zanzibar ambazo ni KMKM, Zimamoto na Uokozi, Mafunzo, JKU na KVZ.

Ilipofika mwaka 2011 tulianza kutengeneza mavazi ya kiraia ikiwemo mashati, viatu, mashuka na sare mbalimbali na kuziuza katika taasisi mbalimbali za serikali na zile za binafsi ikiwemo hoteli, shule na vyuo vikuu kwa gharama nafuu,” amesema.

Anataja ukosefu wa malighafi kuwa ni moja ya changamoto katika utengenezaji wa bidhaa hizo.

Amesema tangu kuanzishwa kwa viwanda hivyo mwitikio umekuwa mkubwa wa watu na taasisi mbalimbali zinazonunua bidhaa hizo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter