Home KILIMOKILIMO BIASHARA Vijana wahamasishwa kuchangamkia fursa za kilimo

Vijana wahamasishwa kuchangamkia fursa za kilimo

0 comment 291 views

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde amewataka vijana nchini Tanzania kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa mbalimbali pamoja na programu za kuwezesha vijana.

Amesema kwa kufanya hivyo, kutatatua changamoto kubwa ya ajira miongoni mwa vijana.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo kwenye Kongamano la Vijana wa Vyuo vikuu na vyuo vya kati lijulikanalo kama ‘University Ladies and Gentlemen Conference’ 2023 lililofanyika Kampasi ya Mazimbu-Chuo cha Kilimo Sokoine Mkoani Morogoro Januari 28, 2023.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye kuhakikisha inachangia upatikanaji wa ajira kwa vijana, imetengeneza mazingira rahisi na kuondoa changamoto zinazowakabili vijana wanaojihusisha na kilimo kwa kuja na programu maalumu kwa vijana inayoitwa ‘Building a Better Tommorow’ (BBT).

Rais Dkt. Samia Suluhu hassan kwa kutambua changamoto zinazowakabili vijana wanaotaka kuwekeza kwenye sekta ya kilimo, ametuelekeza Wizara ya Kilimo tuje na Programu kwajili ya vijana ambapo BBT inalenga vijana na wakina mama,” amesema Mavunde.

Kupitia Program ya BBT Serikali inakwenda kutatua changamoto zinazomkabili kijana kwenye shughuli za kilimo kwa kumuandalia ardhi iliyosajiliwa kwa ajili ya kilimo,upatikanaji wa pembejeo, kupima afya ya udongo ili kufanya kilimo chenye tija, kumtafutia masoko, vilevile kumuandaa kwa mafunzo ya kufanya kilimo biashara katika kituo atamizi cha mafunzo ya Kilimo.

Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo (ASA) Dkt, Sophia Kashenge amewasistiza vijana kuitumia fursa hiyo kufanya kilimo, hata hivyo ameeleza faida za kilimo na namna gani kinaweza kumpatia kipato kijana.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Angellah Kairuki.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo lililoshirikisha vijana zaidi ya 1500 wa Vyuo Vikuu na shule za Sekondari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Angellah Kairuki amewataka vijana kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika shughuli za maendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter