Home Elimu TEHEMA kuboresha ukusanyaji kodi

TEHEMA kuboresha ukusanyaji kodi

0 comment 166 views

Serikali ya Estonia imeahidi kuisaidia Tanzania kuboresha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya ukusanyaji kodi.

Hatua hiyo itasaidia kupiga hatua zaidi katika masuala ya usimazi wa kodi na kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Masuala ya Uchumi na Maendeleo wa Estonia, Mariin Ratnik, katika mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba mjini Doha, Qatar, kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea za kipato cha chini.

Ratnik amesema Serikali yake ipo tayari kuwapokea wataalamu kutoka Tanzania kupata mafunzo ya mifumo ya TEHAMA ya ukusanyaji kodi nchini humo kwa vitendo ili wapate utaalam utakaowasaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake Waziri Nchemba amesema Serikali imepokea rasmi mwaliko wa kuwapeleka wataalamu wa Tanzania kupata mafunzo hivyo wameanza maandalizi ya safari hiyo ambapo mwezi Mei mwaka huu wataalam wanaohusika na masuala ya ukusanyaji kodi watakwenda nchini Estonia kujifunza mifumo mbalimbali ya ukusanyaji kodi.

“Juhudi hizi ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuboresha mifumo ya kodi ili kuwepo na uwazi katika ukusanyaji”, almeeleza Dkt. Mwigulu.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa kuwepo kwa mifumo bora ya ukusanyaji kodi itaongeza uwajibikaji wa watalaam wanaohusika na ukusanyaji kodi.

Aliongeza pia kuwepo kwa mifumo ya pamoja ya ukusanyaji kodi itamsaidia mlipakodi kulipa kodi mara moja katika Taasisi zote zinazohitaji kufanya hivyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter