Home BIASHARAUWEKEZAJI Nishati ya Umeme bado kikwazo kikubwa-TPSF

Nishati ya Umeme bado kikwazo kikubwa-TPSF

0 comment 86 views
Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imedai kuwa changamoto kubwa katika kujenga nchi ya uchumi wa viwanda ni ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika na wa bei nafuu. Akizungumzia juu ya suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye amesema nchi haiwezi kufikia malengo iliyojiwekea endapo upatikanaji wa nishati ya umeme utaendelea kuwa changamoto.

Simbeye amesema hayo jana alipokuwa anasaini mkataba wa maelewano baina ya taasisi hiyo na Oxford Business Group (OBG) ambayo ni taasisi ya utafiti na ushauri wa kimataifa. Ameongeza kuwa uwekezaji katika miradi mikuu ya miundombinu unaofanywa na serikali ya Rais John Magufuli, akitolea mfano mradi wa Stiegler’s Gorge itaboresha upatikanaji wa nishati hii muhimu hapa nchini kwa kiasi kikubwa katika miaka ijayo.

Mbali na hayo, Simbeye pia ameongelea changamoto nyingine kwa makampuni akisema wanapata wakati mgumu kwenye masuala ya mikopo ya riba nafuu kutoka katika taasisi za kifedha na wawekezaji binafsi huku akidai Tanzania inapoteza nafasi kushiriki katika miradi mikubwa kwa sababu ya changamoto hizo kwani wawekezaji huingiwa na hofu.

Naye Mkurugenzi wa Kitaifa wa OBG Ivana Carapic amesema taasisi hiyo itaangalia kwa undani masuala hayo pamoja na mengineyo katika chapisho lao lijalo linalojulikana kama The Report: Tanzania 2017. Wakati huo huo, TPSF itapata fursa ya kuchangia katika ripoti ya kwanza ya taasisi hiyo juu ya fursa za uwekezaji na shughuli za kiuchumi hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter